HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, April 9, 2015

WATU ZAIDI YA 10 WADAIWA KUPOTEZA MAISHA KATIKA AJALI YA MABASI MAWILI YALIYOGONGANA USO KWA USO LEO

 Basi la Ngorika likiwa halitamaniki baada ya kugongana uso kwa uso la basi lingine la Kampuni ya RATCO katika ajali iliyotokea mapema leo kwenye eneo la Kijiji cha Mbweni, Mkata mkoani Tanga. kwa mujibu wa Ripota wetu aliopo eneo la tukio,inadaiwa kwamba mpaka sasa ni Watu kumi wamepoteza maisha katika ajali hiyo, akiwepo Dereva wa Basi la Ratco.Chanzo cha ajali hiyo hakijafahamika mpaka sasa. Globu ya Jamii inafanya jitihada za kumpata Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga kwa maelezo zaidi.
 Hivi ndivyo lionekanavyo Basi la Ratco baada ya kupata ajali hiyo leo.
 Basi la Ngorika lionekanavyo baada ya ajali hiyo.
 Askari Polisi walifika eneo la tukio kwa Wakati ili kuhakikisha usalama unapatikana eneo hilo.
Hivi ndivyo mambo yalivyokuwa, na inasikitisha sana.
 Kiukweli ajali hii ni yakusikitisha na kuhusunisha sana.
 Baada ya ajali ya Mabasi hayo, kulikuwa na gari hii iliyokuwa ikifuatana na moja mabasi hayo, na baada ya mabasi kugongana na gari hii ndogo ikaangukiwa na moja ya mabasi hayo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad