HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, April 9, 2013

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AENDESHA HARAMBEE YA MFUKO WA UDHAMINI WA ELIMU YA JUU WA MWALIMU NYERERE

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati wa Harambee ya Mfuko wa Udhamini wa Elimu ya Juu wa Mwalimu Nyerere, iliyofanyika jana Aprili 8, 2013 katika Ukumbi wa Benki Kuu (BOT) jijini Dar es Salaam. Katika Harambee hiyo zilikusanywa fedha taslimu shilingi milioni 71 na ahadi ya fedha za Kitanzania shilingi milioni 658.
Makamu wa Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi sarafu Dkt. Charles Kimei, baada ya kuinunua sarafu hiyo kwa Sh. milioni 19 katika mnada wa Harambee ya Mfuko wa Udhamini wa Elimu ya Juu wa Mwalimu Nyerere, iliyofanyika jana April 8, 2013 katika Ukumbi wa Benki Kuu (BOT) jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimpongeza Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Reginard Mengi, baada ya kununua sarafu kwa Sh. milioni 20, wakati wa Harambee ya Mfuko wa Udhamini wa Elimu ya Juu wa Mwalimu Nyerere, iliyofanyika jana April 8, 2013 katika Ukumbi wa Benki Kuu (BOT) jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akionyesha moja ya Sarafu iliyopigwa mnada katika harambee ya Mfuko wa Udhamini wa Elimu ya Juu wa Mwalimu Nyerere, iliyofanyika jana Aprili 8, 2013 katika Ukumbi wa Benki Kuu (BOT) jijini Dar es Salaam, ambayo ilinunuliwa na Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Reginard Mengi kwa Sh. milioni 20. Kushoto ni Waziri wa Fedha Dkt. William Mgimwa. Harambee hiyo ilifanyika jana April 8, 2013 katika Ukumbi wa BOT.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa harambee hiyo. Picha na OMR

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad